Jonah 3:5-8

5 aWatu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.

6 bHabari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. 7 cNdipo akatoa tangazo katika Ninawi yote:

“Kwa amri ya mfalme na wakuu wake:

“Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ng’ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa.

8

dBali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao.

Copyright information for SwhKC